MARAFIKI WANAZUNGUMZA WAZI

Je, hatuoni hatari kwamba msisitizo huu wote juu ya urafiki na Mungu mwenye urafiki utadhoofisha heshima ufaao?” Swali hili lilitokea kwa mchungaji katika kongamano la kanisa nililohudhuria hivi majuzi, na nimewasikia wengine wakieleza wasiwasi huo.

Bila shaka, swali hilo linastahili kuchukuliwa kwa uzito, kwa kuwa inaonekana wengi huona ni vigumu kumstahi Mungu akiwa Muumba asiye na kikomo na tena Rafiki mpole. Kama watu walivyodhihirisha milimani Sinai, wakati woga umekwisha, wakati hakuna maonyesho ya ukuu na nguvu, heshima inaonekana kufifia. Maadamu umeme uliangaza na ardhi kutikisika chini ya miguu yao, Waisraeli walikuwa tayari kumuahidi Mungu chochote. Wengine wanaweza kuona utii kama huo wa kutetemeka kama “heshima ifaayo.” Lakini siku chache baada ya ngurumo hiyo kwisha, watu walikuwa wakicheza kwa fujo wakizunguka ile sanamu ya ndama ya dhahabu!1

Maadamu Yesu alilisha umati kimuujiza, kuponya wagonjwa, na kufufua wafu, watu walikuwa tayari kumwabudu na kumtawaza mfalme.

Lakini alipowajibu maadui zake kwaupole wa namna hiyo, alipowatendea wenye dhambi kwa subira na heshima kama hiyo, alipoeleza kwamba ufalme wake hautaletwa kwa nguvu, wakati pale Kalvari aliponyenyekea kwa unyonge sana, wengi wa wafuasi wake ama waliacha au walidhihaki madai yake ya kuwa Mwana wa Mungu.

Yuda alikuwa mmoja wa wale waliodhania neema kuwa udhaifu. Yesu alipopiga magoti ili kuosha miguu yake, Yuda alimdharau kwa sababu ya unyenyekevu wake. Mungu ambaye Yuda angeweza kumheshimu hatawahi kujishushia hadhi namna hiyo.

Ni lipi ambayo inakupa msukumo wa heshima kubwa zaidi: udhihirisho wa kutisha wa nguvu za Mungu kwenye Mlima Sinai au picha ya Muumba mkuu akilia kimya kimya kwenye Mlima wa Mizeituni? Ikiwa hadithi ya pale Mlimani Sinai na hadithi ya Mlimani mzeituni imetuongoza kumwona Mungu kama Mfalme mkuu na Rafiki mwenye neema, basi tumejifunza jinsi ya kumwabudu Mungu kwa aina ya heshima anayotaka – uchaji bila woga na heshima ya marafiki.

Marafiki hao wanaweza kuelewa vizuri zaidi njia za Mungu, kwa kuwa anaweza kuzungumza nao kwa uwazi zaidi. Tofauti na watumishi watiifu, wao wana hamu ya kutaka kujua mengi zaidi kuhusu yule wanayemsifu. Kama marafiki wanapaswa kuwa, hawataki Mungu awe na sifa mbaya- wameonyesha kuwa wanaweza kuaminiwa na habari ambazo wengine wanaweza kutoelewa au hata kutumia vibaya.

Kwao Mungu anaweza kudhihirisha upole wake, bila hatari ya kuudharau kuwa ni udhaifu. Anaweza kuwaambia kwamba yeye hathamini kitu cha juu zaidi kuliko uhuru wao, bila hatari ya kupunguza heshima yao, nidhamu na utaratibu. Anaweza kuonyesha kwamba yeye ni msamaha katika mwili wa binadam, bila hatari kwamba watachukulia dhambi kama jambo lisilo na uzito. Anaweza kuwahakikishia hakuna haja ya kuogopa, bila hatari ya kupunguza heshima na mshangao wao.

Yesu hakuficha maneno yoyote aliponya juu ya hatari za kushiriki habari hizo zenye thamani na wale ambao hawako tayari au wasioweza kuzipokea, au ambao hata wanaweza kuziona kuwa zenye kuudhi.

Alipokaribia mwisho wa maelezo yake ya ajabu kuhusu Mungu katika Mahubiri yake pale Mlimani, alishauri kwa dhati, “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu; wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga na kugeuka na kuwaponda.”2 Ikiwa jambo hilo laonekana kuwa limesistizwa kupita kiasi, jinsi Yesu alivyotendewa katika miaka mitatu iliyofuata yalithibitisha ukweli wa onyo lake.

Hakuna “Lugha ya Siri” Kati ya Marafiki

Wazia ukimsikia Mungu akisema kwamba anaweza kuzungumza nawe kwa njia ambayo hawezi kusema na watu wengine, kwa sababu wewe ni rafiki yake. Musa alipokea pongezi hizo za hali ya juu, nami nimejiuliza jinsi alivyohisi alipomsikiliza Mungu akiwaeleza Mariamu na Haruni kwamba angeweza kusema kwa uwazi zaidi na ndugu yao kuliko hata manabii.

Mariamu na Haruni walikuwa wameonea wivu uhusiano wa pekee ambao Musa alifurahia pamoja na Mungu, ingawa Musa mwenyewe anafafanuliwa kuwa “mnyenyekevu sana kuliko mtu mwingine yeyote duniani.”3 Ninakumbuka nilipokuwa mtoto nilifikiri kwamba ikiwa Musa aliandika mstari huo mwenyewe, hangekuwa mnyenyekevu sana kujivunia unyenyekevu wake mwenyewe! Lakini baadaye nilitambua kwamba inahitaji unyenyekevu mwingi ili kukubali kuwa mpole. Upole hauvutiwi sana au kuaminiwa kwa kiongozi. Wakati wa uchaguzi wa urais, wagombea hawasifu upole na unyenyekevu wao wa kipekee kama jambo la kuwawezesha kuhitimu kushika nyadhifa za juu!

Moja ya shairi la kwanza ambalo mama yangu alinifundisha lilianza kwa maneno, “Yesu mpole, mwenye rehema na mvumilivu, mwangalie mtoto huyu mdogo.” Nilidhani ilikuwa nzuri sana wakati huo. Bado ninafikiri hivyo. Lakini watu wengi ambao Yesu alikuja kuwaeleza juu ya Baba yake walimdharau na kumkataa kwa sababu ya upole wake, kama vile nabii Isaya alivyotabiri.4

Karne nyingi kabla ya haya, Mungu alikuwa amemwambia Musa mpole kwamba siku moja atamwinua nabii maalum kutoka miongoni mwa watu wa Israeli, “nabii kama wewe.”5

Yesu alitambua utabiri huu kuwa ulimrejelea yeye mwenyewe.6 Na lazima Musa alitazama kwa mshangao na kustaajabu zaidi jinsi Mwana wa Mungu alivyoshughulika na kila namna ya watu, na hasa adui zake, kwa unyenyekevu na neema kama hiyo.

Kabla ya Yesu kusulubiwa, Musa alikuja kuzungumza naye kwenye Mlima wa Kugeuzwa Sura (Transfiguration). Nabii Eliya alijiunga nao, na wote watatu – watu wawili na Mungu Muumba wao, ingawa sasa katika umbo la kibinadamu – walizungumza “uso kwa uso,” kama marafiki wakizungumza wao kwa wao. Luka anasema walizungumza kuhusu kukataliwa kikatili na kifo ambacho Yesu alikuwa karibu kuivumilia.7

Ingawa wengi walimdharau Yesu kwa ajili ya upole wake, unadhani Musa aliona haya kusimama pale na Bwana wake? Ni heshima iliyoje kutambuliwa na “Yesu mpole, mwenye rehema na mvumilivu!” Musa hakuwa ameona aibu kujieleza katika kitabu cha Hesabu kuwa mpole na mnyenyekevu zaidi “kuliko mtu mwingine yeyote duniani.” Kuwa mtu wa aina hiyo ni kuwa kama Mungu.

Hata hivyo, ingeonekana kwamba sifa hizo za Musa hazikuwa zimefanya ndugu na dada yake wamuaheshimiu. Mungu aliwaita wote watatu mbele zake. Haruni na Miriamu waliamriwa wasogee mbele. Mungu akasema, Sikieni maneno yangu.

Wakati kuna manabii kati yenu,
Mimi, Bwana najijulisha kwao katika maono;
Ninazungumza nao katika ndoto.
Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu Musa;
amekabidhiwa nyumba yangu yote.
Ninasema Naye uso kwa uso, kwa uwazi, si kwa mafumbo;
naye huona umbo la Bwana.
Mbona basi hamkuogopa kusema juu ya mtumishi wangu Musa?8

(Tafsiri ya King James Version inatafsiri neno la Kiebrania la “vitendawili”(riddles) kama ” Lugha ya siri.”)

Ona kwamba bado Mungu anamwita rafiki yake Musa kama mtumishi wake. Katika pindi fulani mapema Mungu alifafanuliwa kuwa akizungumza na Musa “uso kwa uso, kama mtu asemavyo na rafiki.”9 Lakini urafiki na Mungu sio mwisho wa huduma. Yesu mwenyewe aliweka kielelezo cha kuwa rafiki anayetumika.

Kuzungumza kwa Uwazi juu ya Baba

Muda mfupi baada ya Yesu kutoa pendekezo la urafiki lililorekodiwa katika Yohana 15:15, aliwaambia wanafunzi kwamba hivi karibuni angeanza kuzungumza nao kwa uwazi zaidi juu ya Baba. Alieleza kwamba hadi wakati huu alikuwa akizungumza nao kwa tamathali za semi, mafumbo, hekaya- “lugha ya siri” ambayo hakuwa na haja ya kutumia na rafiki yake Musa. “Saa inakuja ambayo sitasema nanyi tena kwa mafumbo, bali nitawaambia waziwazi juu ya Baba.”10

Ilichukua muda gani hadi wakati huo kufika? Wanafunzi inaonekana walifikiri, mara moja. Baada ya Yesu kumaliza maneno mafupi lakini ya maana sana kumhusu Baba, wanafunzi walijibu, “Naam, sasa wanena waziwazi, si kwa mfano wo wote!11 Linganisha maneno ya Bwana muda mfupi tu baadaye, akitabiri jinsi wanafunzi wangemwacha, “Saa inakuja, hakika imefika…”12

Yesu alitoa kauli yake wazi katika lugha ya Kiaramu. Yohana aliitafsiri kwa Kigiriki. Tunaisoma katika tafsiri za tafsiri ya Yohana. Lakini hatuna haja ya kuwa na wasiwasi kwamba katika utafsiri huu wote, jambo la maana asili kinaweza kuwa kimefichwa.

Matoleo mengi ya kifungu hiki yanasoma sawa. Hapa kuna Kiingereza cha New International Version:

Ingawa nimekuwa nikisema kwa mafumbo, saa inakuja ambapo sitatumia tena lugha ya namna hii bali nitawaambia waziwazi juu ya Baba yangu. Siku hiyo mtaomba kwa jina langu. Sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu. Hapana, Baba mwenyewe anawapenda ninyi kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nilitoka kwa Mungu. nalitoka kwa Baba na niliingia ulimwenguni; sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba.13

Ninafurahia hasa mstari wa 27 la toleo la Knox. “Kwa sababu Baba mwenyewe ni rafiki yenu, kwa vile mmekuwa marafiki zangu …” Monsinyo Knox alitafsiri kutoka kwa tafsiri ya Kilatini ya tafsiri ya Yohana ya Kigiriki. Lakini katika Kilatini na Kigiriki, maneno yanayomaanisha “upendo” na “rafiki” yanatoka kwenye mzizi mmoja wa msingi.

Katika kile Yesu alichosema kuhusu Baba, je, kuna jambo lolote linaloonekana kuelezwa kwa uwazi zaidi na kutumia mafumbo kidogo zaidi kuliko hapo awali? Ninapata maneno rahisi tu, ambayo yanaweza kutumia Kiingereza rahisi, “Sisemi nanyi kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu, kwa maana Baba anawapenda mwenyewe.”

Goodspeed inatafsiri kifungu hiki, “Siahidi kuwaombea kwa Baba, kwa maana Baba anawapenda ninyi.”

Wakiwa marafiki wa Mungu mwenye urafiki, wanafunzi walitiwa moyo kuwasilisha maombi yao wenyewe moja kwa moja kwa Baba. Haikuwa lazima kwa Yesu kuwafanyia hivi.

Hata hivyo, walipaswa “ombeni kwa jina langu,” Yesu alisema. Hilo halikumaanisha kwamba ikiwa Mungu hangesikia jina la Mwana wake, hangekuwa tayari kutimiza maombi yake. Kutajwa kwa jina la Yesu kunaonyesha utambuzi wa shukrani kwamba ikiwa Mwana wa Mungu hakuwa ametuonyesha ukweli kuhusu Baba yake, hatukujua jinsi tungeweza kumkaribia. Huenda hata hatutaki.

Kwa maana hii, kwa hakika tumehitaji mtu wa “kupatanisha,” “kuombea,” “kuingilia kati,” maneno yote yenye msingi wa Kilatini yakimaanisha kwa mtiririko huo “kuwa katikati,” “kwenda kati,” “kuingia kati. ” Kila mara tunaposali katika jina la Yesu, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Kristo Mpatanishi wetu, aliyekuja kuziba pengo kati yetu na Mungu na kutuletea ukweli kuhusu Baba yetu wa mbinguni mwenye upendo.

Kwa sababu ya Yesu, tunajua kwamba tunaweza kuzungumza na Baba yetu wa mbinguni “kama mtu asemavyo na rafiki.” Hakuna uhitaji wa kuwa na rafiki mwingine kati, kwa maana Mungu mwenyewe ndiye Rafiki yetu.

Kati ya yote ambayo Yesu angeweza kuweka wazi juu ya Baba yake, kwa nini alichagua habari hii hasa, na kwa nini wakati huu kabla ya kusulubishwa kwake? Je, hili lilikuwa jambo ambalo wanafunzi wangehitaji hasa kukumbuka waliposhuhudia matukio ya saa chache zilizo fuata? Je, lilikuwa jambo ambalo wanafunzi walihitaji kujua waziwazi, wasije wakaelewa vibaya maana ya kifo chake kama dhabihu?

Siri ya Kutoweka “Sio”

Kwa kushangaza, si kila mtu anafurahi kusikia taarifa hii ya wazi kuhusu Baba iliyorekodiwa katika Yohana 16. Kwa hakika, niliwahi kumsikia mhudumu mmoja akilishutumu kama “uzushi mbaya sana.” “Ikiwa Yesu hatuombei kwa Baba,” aliendelea, “hatuna tumaini la kuokolewa.”

Nina hakika mhudumu huyu hakutambua kwamba alikuwa akiyahukumu maneno ya Kristo mwenyewe. Kwa hiyo kwa uungwana wote ni lazima nionyeshe kwamba amezoea, kama wengine wengi, kusoma Yohana 6:26 bila neno muhimu zaidi “sio.” Yesu alisema, “Sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu.” Lakini kwa wasomaji wengi, “si” imetoweka kwa namna fulani.

Katika hafla nyingi za hadhara, na wakati mwingine hata kwa kuchapishwa, nimeona mstari huu ukinukuliwa – bila “si” – kama ahadi kwamba Yesu hakika atamsihi Baba kwa ajili yetu. Wengine wameonyesha mshangao mkubwa wakati umakini wao unapoitajiwa kwa neno lililokosekana.

Nimesikia hata wahubiri wakikiri kwamba, kama “sio” ni mali, hawajui la kufanya na andiko hili, Wengine wanalipuuza tu.

Mwalimu mmoja alieleza, “Kwa kuwa sisi sote tunajua kwamba Kristo kwa kweli anafanya maombezi na Baba, Yohana 16:26 ni kitendawili kigumu.” Alimaanisha hili, bila shaka, na “si” ya Bwana bado iko mahali. Lakini Yesu hakusema kauli hii ilikuwa ngumu. Alisema ni wazi na pia dhahiri!

Nafasi ya Kuuliza Maswali

Wanafunzi walikosa nafasi nyingine ya kutenda kama marafiki kama walivyokuwa wamealikwa, na kuuliza maswali jinsi marafiki wanavyofanya. Wangeweza kumwuliza Yesu ikiwa kweli alimaanisha yale ambayo alikuwa ametoka kuwaambia.

“Je, unasema kwamba hakuna haja ya wewe kutuombea Baba? Basi. Kwa nini Musa aliagizwa kuweka utaratibu mzima wa ukuhani pale Sinai?”

Je, haikuwa kazi maalum ya kuhani mkuu kuomba Mungu kwa ajili ya wenye dhambi?14

“Je, haikumbidi Musa kumsihi Mungu ili asimwage ghadhabu yake juu ya watu wapotovu?”

“Je, Musa mwenyewe hakutoa taarifa kwamba alifanikiwa kumshawishi Mungu abadili mawazo yake?”

Wanafunzi wangeweza kuelekeza uangalifu wa Yesu kwenye maneno yenyewe ya Maandiko: “Musa akamsihi Bwana, Mungu wake, akasema… Geuka katika ghadhabu yako kali; … Na Bwana akabadili mpango Wake juu ya maafa aliyopanga kuwaletea watu Wake.”15

“Je, unatuambia, Bwana, kwamba hata Musa hakuelewa?”

Katika wakati wetu, tukiwa na faida ya kuwa tumesoma kitabu cha Waebrania, tunaweza kuuliza swali lingine: “Yesu, ikiwa kazi ya kuhani mkuu iliwakilisha kazi hiyo hiyo uliyokuja kuifanya, nawe umeendelea kuifanya tangu urudi mbele za Baba – kwa nini ungesema kwamba hakuna haja ya wewe kufanya maombezi kwa Mungu kwa niaba yetu? Kwanaini basis marafiki wa Yesu Yohana na Paulo wanamtaja kama Wakili anayetetea kesi yetu katika mahakama za mbinguni katika barua zao za Agano Jipya kama?16 Je, hata wao hawakuelewa? Je, labda Yohana alishangazwa kukusikia ukiendelea kumwomba Baba kufanya mambo kwa ajili ya wanafunzi, mara baada ya wewe kusema kwamba ‘hauta waombea?”17

Laiti Yohana angemwomba Yesu amsaidie kuelewa maana ya kauli yake ya wazi kuhusu Baba. Ndipo Yohana angeandika jibu lisilokadirika, na tunaweza kuwa tunalisoma leo. Walakini, kutoka kwa Maandiko mengine, tunaweza kuwa na wazo fulani la jinsi Bwana angeelezea jambo hili.

“Sijaja kumpinga Musa”

Huenda Yesu alianza kwa kurudia maneno aliyowaambia wachambuzi waliomshtaki kwamba anapinga mafundisho ya Maandiko matakatifu. “Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kukamilisha na kutimiliza.”18

Kisha, kama ilivyokuwa desturi yake kujibu maswali hayo, huenda Yesu alifuatilia historia ya wazo zima la kwamba watoto wa Mungu walihitaji mtu wa kusimama kati yao na Baba yao wa mbinguni. Angeweza kuwakumbusha wanafunzi jinsi Mungu alishuka Mlimani Sinai ili kuzungumza na watu wake, juu ya hatua alizopaswa kuchukua ili kupata usikivu wao, jinsi kwa hofu watu walivyomsihi Musa asimruhusu Mungu kusema nao moja kwa moja wasije wakaangamizwa.

Wewe, Musa, sema nasi, nasi tutasikia; lakini usimwache Mungu aseme nasi, tusije tukafa.19

“Unaona,” Yesu angeweza kuendelea, “ni watu waliotaka mtu fulani katikati, mtu ambaye walielewa kuwa rafiki ya Mungu, ambaye angeweza kusimama kati yao na Mungu ambaye walimwogopa sana.

“Lakini ninyi wanafunzi mnajua ya kuwa mimi ndiye niliyekuwa kule Mlimani Sinai. Je, kuna yeyote kati yenu anayeniogopa? Nimewauliza muwe marafiki zangu. Mnajua ni salama kwenu kuketi na kuzungumza nami kwa uwazi namna hii.”

Sikutaka Mtu Yeyote Kati

Kisha Yesu angeweza kuendelea, kwa huzuni, “Ningalipenda kuzungumza hivi na watu wangu kule nyikani. hawakunijua mimi kama ninyi, kwanza hawakuwa na heshima, kisha waliogopa sana. Sikuweza kuwaamuru wasiogope. Kama ninyi wanafunzi hakika mnapaswa kuelewa, uaminifu na urafiki hauwezi kuamriwa. walinifahamu vyema, nilikubali kuwa Musa anaweza kuwa mpatanishi, hawakumuogopa na wala hakuniogopa.

“Bila shaka hakukuwa na mtu kati yangu na Musa, alinifahamu sana na alikuwa rafiki yangu, hakukuwa na mtu yeyote kati yangu na rafiki yangu wa zamani Ibrahimu alipozungumza waziwazi kuhusu mipango yangu kwa watu wa Sodoma. Hakukuwa na mtu kati yangu na Ayubu alipojisikia huru kueleza hisia zake kwa nguvu sana.Washauri wake walifikiri ningekasirika, lakini kwa kweli niliheshimiwa kwa uaminifu wake.

“Na sasa,” Yesu anaweza kuwa alihitimisha, “nimekuja binafsi kuwa mmoja kati – kama nilivyomwambia Musa ningefanya. Wengi wanaweza kutoelewa kusudi langu la kuja. Wengi wanaweza hata kumshukuru Mungu kwa dhati kwa kunituma mimi, mimi niliye mpole, kusimama kati yao na Baba yao wa mbinguni aliyekasirika – kana kwamba mimi ni mpole kuliko yeye.

“Lakini mnajua mimi ni nani. Mmeona kwamba Isaya alikuwa sahihi alipotabiri kwamba Mfalme wa amani atakuwa Mungu.20 Sasa niambieni ukweli, wanafunzi wangu. Je! mnahitaji mtu yeyote kuwalinda kutoka kwangu? Hamuna haja ya mtu yeyote kuwalinda kutoka kwa Baba. Ulipokuwa unafanya vibaya sana wakati wa chakula cha Pasaka, je, kulikuwa na mtu yeyote kati yenu na Mungu nilipowaosha miguu yenu michafu? Niliposha miguu ya Yuda, hapakuwa na mtu kati yake na Mungu wake.

“Nimewaambia kwa uwazi na kwa udhahiri niwezavyo kwamba Baba anawapenda kama mimi. Yeye ni wa kirafiki na mwenye kusamehe kama ninavyotumaini kwamba mumenipata kuwa. Hata angekuwa tayari kupiga magoti na kutusamehe na kuosha miguu yetu michafu.

“Lakini sasa lazima niende kusulubishwa. Nataka muwe pamoja nami pale Kalvari. Nataka munitazame nikifa. Labda itawasaidia kuelewa kwa uwazi zaidi kile ambacho nimekuwa nikijaribu kuwambia juu ya Baba.”

Cha kusikitisha ni kwamba, kati ya wale wanafunzi kumi na wawili, Yohana ndiye pekee aliyekuwa hapo.

Lakini aliandika yale aliyosikia na kuona.

Nani Anatupenda Zaidi-Yesu au Baba?

Katika ibada ya familia miaka mingi iliyopita, binti yangu mdogo alipokuwa na umri wa miaka sita tu, tulikuwa tukisoma pamoja hadithi ya watoto kutoka katika gazeti la Kikristo. Ilisimulia sana jinsi Yesu anavyosimama mbele ya Baba yake na kumwomba awasamehe—hasa watoto wadogo ambao hawajakuwa wema!

“Baba,” alikatiza Alice, huku uso wake ukiwa na wasiwasi, “inamaanisha kwamba Mungu hatupendi kama Yesu anavyotupenda? Ilionekana wazi kwake kwamba aliyetuombea lazima awe na upendo zaidi kuliko yule aliyelazimika kuombwa.

Ibada ilikuwa ndefu kidogo jioni hiyo. Msichana mdogo alikuwa amejihisi huru kuuliza swali muhimu sana kumhusu Mungu. Na kweli alitaka kuelewa.

Nilimweleza kisa cha kile ambacho Yesu alijaribu kukifanya kwa uwazi na kuwa dhahiri kwa wanafunzi wake katika chumba cha juu.

Sasa Alice anawaeleza wajukuu wangu kwamba Mungu anawapenda kama vile Yesu anavyowapenda.

Nukuu

  1. Ona Kutoka 32.
  2. Mathayo 7:6, NRSV.
  3. Hesabu 12:3, NRSV.
  4. Ona Isaya 53:3,7.
  5. Ona Kumbukumbu la Torati 18:15-18.
  6. Ona Luka 24:27,44; ona pia Matendo 3:17-26 .
  7. Ona Luka 9:28,36; ona pia Mathayo 17:1-8, Marko 9:2-8.
  8. Hesabu 12:6-8, NRSV.
  9. Kutoka 33:11 , NRSV.
  10. Yohana 16:25 , NRSV.
  11. Yohana 16:29 , NRSV.
  12. Yohana 16:32 , NRSV.
  13. Yohana 16:25-28, NIV.
  14. Ona Mambo ya Walawi 16.
  15. Kutoka 32:11-14 , NRSV.
  16. Ona l Yohana 2:1; Warumi 8:34.
  17. Ona Yohana 17:6-26.
  18. Ona Mathayo 5:17.
  19. Ona Kutoka 20:18,19.
  20. Ona Isaya 9:6.