Graham Maxwell
Limetafsiri kutoka Kiingereza hadi Kiswahili na Mary Mercy Kobimbo
Maandishi © 1992 Graham Maxwell. Haki zote zimehifadhiwa.
Pine Knoll Publications, Redlands, California
Dibaji
Je, umewahi kusikia mfalme akiwaambia watu wake kwamba wao si watumishi wake tena? Badala yake, wakikubali, atawaamini kuwa marafiki wanaotegemeka. Mfalme anataka kila mtu ajue kwamba hataki watumishi wanaomtii bila kufikiria. Afadhali angepata ushirikiano huru na wa busara. Ili aweze kufanya hivyo, anaahidi kuwafahamisha wananchi wake kuhusu jinsi serikali yake inavyofanya kazi.
Biblia inarekodi kwamba Yesu aliwatolea wanafunzi wake offa hilo la ajabu kabla hajarudi mbinguni ili kuanza tena mamlaka yake kamili ya kifalme. Yohana alikuwa pamoja na Yesu alipotoa ofa hili, na aliliandika katika Injili yake – katika sura ya kumi na tano na mstari wa kumi na tano. “Siwaiti tena watumishi wangu,” Yesu alisema, “maana watumishi hufanya tu yale wanayoambiwa. Afadhali nawaita ninyi rafiki zangu, kwa maana nataka mfahamu.”
Yule ambaye Biblia inamtaja kuwa “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana” anapendelea kutuchukulia sio watumishi, bali kama marafiki. Kwangu mimi, hii ndiyo habari njema iliyo bora kuliko zote tunazoziita Injili. Fikiria hili linamaanisha nini kuhusu tabia ya Mungu na jinsi ingekuwa kuishi milele na Mungu kama huyo.
Katika karibu miaka hamsini ya mafundisho ya Biblia ya chuo kikuu, imekuwa furaha yangu kuu kuendesha kozi ya mwaka mzima ambayo inahusisha kusoma kila moja ya vitabu sitini na sita katika Agano la Kale na Agano Jipya.1 Kusudi ni kujifunza jinsi ya kuitazama Biblia kwa ujumla na jinsi sehemu zake zote zinavyohusiana na somo moja muhimu zaidi, ambalo ni ukweli kumhusu Mungu. Ninapokumbuka safari 135 kama hizi kupitia majimbo yote sitini na sita. kuna kifungu kimoja ambacho kinaonekana wazi zaidi kuwa kinafunua ukweli muhimu zaidi kuhusu Mungu – hili ni ufunguo wa kuelewa Maandiko mengine yote na mpango wa Mungu wa kurejesha amani katika ulimwengu wake. Ofa hii ya urafiki iliyorekodiwa katika Yohana 15:15.
Lengo la kitabu hiki, Watumishi au Marafiki? ni kuzingatia jinsi upendeleo wa wazi wa Mungu wa uhuru wa kuelewa urafiki una matokeo makubwa na ya kutamanika sana kwa baadhi ya waumini kuliko huduma ya kunyenyekea tu.
Nukuu
- Vile vitabu “Sitini na sita” vinajumuisha vitabu 39 ambavyo Wakristo na Wayahudi wengi wanakubali kuwa ni vya kweli, na vile vitabu 27 vya Agano Jipya ambavyo Wakristo wengi wanakubali ni vya kweli.
Yaliyomo
- 1JE, UNAOGOPA KUKUTANA NA MUNGU?
- 2NAPENDA MWE RAFIKI ZANGU
- 3HAKUNA URAFIKI BILA KUAMINIANA
- 4UAMINIFU HAUWEZI KUAMRISHWA
- 5KUWA MAKINI UNACHOKIAMINI
- 6MARAFIKI WANAZUNGUMZA WAZI
- 7URAFIKI NA MATUMIZI YA MUNGU YA SHERIA
- 8JINSI WATUMISHI NA MARAFIKI WAONAVYO DHAMBI NA WOKOVU
- 9NI RAFIKI WAKO WA KARIBU TU NDIYE ANGEKUONYESHA
- 10UHURU WA URAFIKI
- 11URAFIKI NA MAPAMBANO NA DHAMBI
- 12URAFIKI NA MAANA YA UPATANISHO
- 13TUMEPIGA KAMBI HAPA MLIMANI KWA MUDA MREFU SANA
- 14MARAFIKI WA MUNGU RAFIKI
- 15Mwandishi
