Zaidi ya miaka elfu moja mia tisa imepita tangu Yesu awatume wafuasi wake waipeleke injili ulimwenguni kote. Pia alisema, hayo yakishatimika, mwisho utakuja (Mathayo 24:14).
Ukweli ambao mwana wa Mungu alikuja kuufunua haukupaswa kulindwa kama siri inayojulikana tu na wachache waliobahatika. Ingawa baadhi ya dini maarufu siku zile za Yesu zilizojulikana kama Siri, zilijengwa juu ya habari takatifu iliyofunuliwa tu kwa wale ambao walikuwa wamepitia ibada maalum za uanzishaji.
Lakini “injili” inamaanisha “habari njema,” na kwa hivyo ilipaswa kutangazwa hadharani. Yesu aliagiza injili ipewe usambazaji mkubwa zaidi, hata mpaka “mwisho wa dunia” (Matendo 1: 8), kwa “mataifa yote” (Matt 28:19), “kwa viumbe vyote” (Marko 16:15). Ukweli ulipaswa kufika umbali ule uwongo wa Shetani ulikuwa umefikia.
Kikundi kidogo cha waumini wa Kikristo kilianza kwa ujasiri kutekeleza jukumu hili kubwa. Walitarajia hata kuwa wangeukamilisha kwa muda mfupi sana. Si Yesu alikuwa ameonyesha kwamba atarudi hivi karibuni? Hakuwa amewaonya wawe macho kila wakati wasije wakakosa kuwa tayari kwa kurudi kwake, na kisha kushangazwa? Waamini wengine katika Thesalonike hata waliacha kufanya kazi, kwa imani isiyo sahihi kwamba mwisho ulikuwa tayari umefika. Ilimbidi Paulo awajulishe kwamba bado kulikuwa na matukio muhimu ambayo yangetukia kabla Kristo hajarudi (2 Wathesalonike 2:1-12; 3:6-13).
Lakini kizazi kizima kilipita, na bado Bwana alikuwa hajaja. Sasa ni Yohana pekee aliyesalia kati ya mitume kumi na wawili wa awali, na alifungwa kwenye Kisiwa cha upweke cha Patmo. Je, kulikuwa na tatizo? Habari Njema ilipokelewa vyema na wengi. Lakini pia ilikuwa imesababisha upinzani mkali na nyakati fulani wenye jeuri. Wakristo wengi hata walikuwa wameuawa na watu wale wale waliokuwa wakijaribu kuwasaidia.
Lakini, kwa uzito zaidi, baadhi ya waumini walikuwa wameanza kutilia shaka ukweli wa Habari Njema waliyokuwa wakijaribu kueneza. Baadhi walikuwa sasa hata wanakana kwamba Mwana wa Mungu alikuwa kweli amekuja katika umbo la binadamu kuleta ukweli kuhusu Baba yake (2 Yohana 7).
Wakati huo muhimu Mungu alituma ujumbe mwingine wa kutia moyo na maelezo. Kwa Yohana mfungwa mzee akiwa kwenye Kisiwa cha Patmo, Mungu alituma ujumbe ulionakiliwa katika kitabu cha mwisho cha Agano Jipya. Yohana alieleleza ujumbe huo kuwa ni “ufunuo wa Yesu Kristo, ambaye Mungu alimpa awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kutokea hivi karibuni” (Ufunuo 1: 1).
Ujumbe huu uliwashauri Wakristo wawe na mtazamo mkubwa wa maisha badala ya kuzingatia tu ugumu wa wakati huu uliomo. Kila muumini lazima aelewe kwamba amehusika kikamilifu katika pambano kuu kati ya Kristo na Shetani ambao unaohusisha ulimwengu wote.
Kwa mara ya kwanza Bibilia inataja vita vilivyokuwa zamani huko juu mbinguni na kiwango cha ushawishi wa Shetani kati ya malaika (ona Ufunuo 12). Mkristo ni lazima ajifunze kuona utume wake maalum kwa kuzingatia pambano hili kubwa. Ili itakapoonekana kuwa kazi ya kueneza injili haitafaulu na kuja kwa Kristo mara ya pili kumecheleweshwa kwa muda usiojulikana, aje kukumbuka hili pambano kuu na vyote ambavyo Mungu ametimiza hadi sasa.
Atakumbuka jinsi kwa nyakati zote Mungu amefanya kazi kwa uvumilivu kufunua ukweli juu yake mwenyewe—na bado anafanya kazi kwa uvumilivu ili kushawishi jamii ya binadamu. Kisha kuvunjika moyo kwa ajili ya kuchelewa kwa Kristo kutageuka kuwa shukrani na kupendezwa na neema ya Mungu isiyo na kipimo, na muumini atakuwa yuko tayari kusubiri.
Zaidi ya hayo, Kitabu cha Ufunuo wa Yohana kinazungumza juu ya hasira ya Shetani kwa wale ambao wanathubutu kuzuia juhudi zake za kuudanganya ulimwengu. Anapojaribu kugeuza watu wamwasi Mungu, anakasirika kusikia ushuhuda wa wale ambao bado wanachagua “kutii amri za Mungu na ni waaminifu kwa ukweli uliofunuliwa na Yesu”(Ufunuo 12:17, GNT). Hii inapaswa kuwasaidia waumini kuelewa ni kwa nini juhudi zao za kufundisha ukweli zimechochea upinzani mkali.
Kisha kwa kutazamia siku zijazo, Ufunuo 13 unatabiri jitihada kuu la Shetani la mwisho kwa njia ya udanganyifu, muujiza, utumiaji wa nguvu kunyamazisha ukweli na kujizindua kama Mungu.Mapambano ni makali sana hivyo Yohana anakatiza maelezo yake nakutuambia, “Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani” (Ufunuo 13:10, GNT).
Katika Ufunuo sura ya 14 mtume anaendelea kutuelezea kundi hili la watu wa Mungu ambao bado wanapinga uwongo wa Shetani hadi mwisho. Inatajwa hasa juu yao kwamba “hakuna uongo uliopatikana kinywani mwao” (Ufunuo 14: 5). Hata wakihatarisha maisha yao wanakataa kujiunga na ulimwengu unaogeuka kutoka kwa Mungu wa ukweli na kuabudu yule Kristo alikuwa amemwita “baba wa uwongo” (Yohana 8:44). Badala yake, wanaendelea “kushika amri za Mungu na kubaki waaminifu kwa Yesu” (Ufunuo 14:12, NEB).
Mashindano yakiwa yanaelekea kilele chake, waaminifu wa Mungu hawatakuwa tu wakingojea ahadi ya kurudi kwa Bwana wao bila kushugulika. La! Hawatamwachia adui nafasi ashawishi ulimwengu kwa urahisi! Badala yake, watatia juhudi maradufu kukamilisha agizo walilopewa la kueneza ukweli kufikia pembe zote za dunia.
Tena katika lugha ya mfano ya Kitabu cha Ufunuo, Yohana anaandika yakuwa anaona juhudi kubwa ya mwisho ya kueneza injili ikiwakilishwa na malaika wakileta ujumbe wa haraka kutoka mbinguni. Katika Ufunuo sura ya 14 anataja hasa malaika watatu.
Wa kwanza wa hawa Yohana aliona “akiruka juu angani, na ujumbe wa milele wa Habari Njema kutangaza kwa watu wa dunia, kwa kila kabila, lugha, na taifa ……. [Malaika] alisema kwa sauti kubwa , ‘Mheshimu Mungu na msifu ukuu wake!’ Kwa maana wakati umewadia wa kuwahukumu wanadamu. Mwabuduni yeye aliyezifanya mbingu, na nchi, na bahari, na chemchemi za maji! (Ufunuo 14: 6, 7, GNT). “Malaika wa pili akamfuata yule wa kwanza, akisema, Ameanguka! Babeli kubwa imeanguka! ” (Ufunuo 14: 8, GNT). Upinzani wa Mungu umeanguka, kwa ufisadi na kushindwa!
Malaika wa tatu aliwafuata wale wawili wa kwanza na kwa lugha dhahiri alionya juu ya matokeo mabaya ya kuamini uwongo wa Shetani na kujiunga naye katika kumwasi Mungu. Kwa mara nyingine kuna wito wa “uvumilivu kwa watu wa Mungu, wale wanaotii amri za Mungu na ni waaminifu kwa Yesu” (Ufunuo 12:14, GNT).
Jumbe hizi tatu katika mazingira yao, zinaonekana kujumlisha ujumbe wa Mungu wa mwaliko wa mwisho na onyo kwa ulimwengu wetu. Walakini ujumbe huo sio mpya. Habari Njema ya malaika wa kwanza inaelezewa kuwa ni ya milele, isiyo na mwisho. Imekuwa ndiyo ukweli daima.
Ilikuwa kweli katika umilele, hata kabla ya Lusifa kuanza kusambaza uwongo wake. Ni huo ukweli ambao umeshikilia uaminifu wa watoto wengi wa Mungu ulimwenguni kote. Na itabaki kuwa ukweli katika enzi za milele usio na mwisho, ukweli ambao ndio msingi wa uhuru tulilopewa kumtegemea Mungu. Lakini, hii ukweli, injili ya milele na Habari Njema ni nini haswa?
