Tazama, jinsi ilivyo vema,
na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja!
– Swahili Revised Union Version
Ni jambo zuri na la kupendeza sana
ndugu kuishi pamoja kwa umoja!
– Biblia Habari Njema.
Jinsi gani ilivyo vyema na kufurahisa kwa watu wote kuishi pamoja kama ndugu!
-The Jerusalem Bible
Je! Kuna kitu chochote Kinachotamanika zaidi kuliko watu kuishi pamoja kama jinsi ilivyoelezewa katika Zaburi 133:1? Mimi sijui hali yeyote ya furaha kuu kuliko kuwa miongoni mwa marafiki wa kuaminika na wanaoaminiana, wote wakifanya kazi kwa ajili ya masilahi ya kila mtu mwingine, bila wivu au kutokuaminiana, kila mtu akiwazia vizuri zaidi tabia na maneno ya mwenzake.
Umoja wa aina hii na nia njema vinaweza kuwepo tu pale ambapo kuna uaminifu kamili na uwezekano wa kuaminiwa, upendo wa pande zote, na kuheshimiana. Lakini Biblia inaonyesha picha ya jamii yote ya binadam ikiwa imenaswa katika mtandao mkubwa wa kutokuaminiana. Haya yote ni sehemu ya mgogoro ya kuaminika ulimwenguni kote wenye mizizi ya swala la kuaminika kwa Mungu mwenyewe.
Mungu wetu asiye na mwisho ameshtumiwa kwa madai ya kutokuaminika. Lakini Mungu amejibu shtaka hili kwa njia ya uthibitisho wenye kusadikisha zaidi kwamba yeye anastahili kabisa imani yetu.
Biblia ni rekodi ya dhihirisho ndefu tena ya gharama kubwa inayoonyesha uaminifu wa Mungu. Ikiwa uaminifu ungeweza kupatikana kwa madai au himizo tu, Biblia ingekuwa kitabu tofauti kabisa. Lakini madai ya uaminifu hayana thamani pasipo kuwa na uaminifu wa yule anayetoa madai hayo. Kwa hivyo, hata wakati mtu ameshtumiwa kwa uwongo, kukubali madai au kukanusha tu hayathibitishi chochote. Uaminifu huthibitishwa na kusadikishwa kwa maonyesho ya vitendo vilivyotokea katika mazingira mbali mbali kwa kipindi kirefu.
Ijapokuwa Biblia inaeleweka kwa ujumla kuwa inashughulikia sana mpango wa Mungu wa kuwaokoa wenye dhambi, swala kuu zaidi linaloshughulikiwa katika kurasa za Maandiko Matakatifu ni ukweli na uaminifu wa Mungu muumba mwenyewe, kwa njia ya swali ambalo imewasilishwa na kusikika wazi ulimwengu wote ukitazama. Je, Mungu anaweza kuaminika? Jibu lake Mungu kwa swali hili linawalenga wao nasi sote.
Kitabu hiki kinazingatia kwa kifupi maswala na majibu kwenye pambano kuu juu ya tabia ya Mungu. Mungu, ambaye ni mwalimu mwenye fadhili na ushawishi mkuu, anatualika wazi kuchunguza ushahidi, kwa kusoma rekodi yote – ya vitabu vyote sitini na sita vya Biblia na kufanya uamuzi wetu wenyewe ikiwa ukweli uko upande wake Mungu na ikiwa anastahili uaminifu wetu.
Biblia huzungumza juu ya umoja maalum ambao upo kati ya wale ambao wamekombolewa na kumrudia Mungu kwa imani. Kwa kumwamini na kumpenda huyu Mungu, wanajikuta wanaweza kuaminiana na kuheshimiana. Vivyo wanapata uzoefu wa “jinsi ilivyo nzuri na kupendeza, watu wa Mungu wakiishi pamoja kwa maelewano!”
